Publication

Our Resources

UKIMWI NI NINI?

Resource
MASWALI YANAYO ULIZWA KUHUSU VVU
NA UKIMWI
Virusi vya UKIMWI (VVU) ni nini?
Ni virusi vinavyo shambulia kinga ya mwili na kusababisha ugonjwa wa UKIMWI.
UKIMWI NI NINI?
Neno UKIMWI ni kifupisho cha Upungufu wa
Kinga Mwilini
U - Upungufu wa
KI - Kinga
MWI - Mwilini
Kuna uhusiano gani kati ya VVU na UKIMWI?
Virusi Vya UKIMWI vinapoingia katika
mwili wa binadamu hushambulia chembe
chembe nyeupe za damu hivyo kusababisha
mwili kukosa kinga yake ya asili dhidi ya
magonjwa. Mwili ukipungukiwa na kinga ya
asili hushambuliwa kwa urahisi na magonjwa
mbalimbali, hivyo hali hiyo huitwa UKIMWI .